
Vipindi vya Redio Vatican vinaweza kupatikana kwa kuombwa kutoka sehemu zingine zenye Mashirika ya utangazaji kwa njia ya Redio.
Kwa Redio Katoliki za Afrika , Radio Vatican , ikishirikiana na SIGNIS ( Shirika Katoliki kwa Ajili ya Mawasiliano Jamii), wameandaa utaratibu maalum wa kusambaza bila malipo , vipindi barani Afrika, shukurani kwa mtandao wa Kisetilite wa V-Sat.
Mfumo wa V-Sat, huruhusu hata kiwango kidogo sana cha sauti kuchukuliwa , na hivyo sauti za Redio Vatican, huchukuliwa na kuunganishwa katika Internet kupitia Satellite. Kupitia mfumo huohuo, wakati wa Ibada zinazooongozwa na Papa, huwezekana kutoa sauti za watoaji wa maoni moja kwa moja , kwa lugha ya Kifaransa, Kiingereza na Kireno.
Kwa wanaopenda kuunganishwa katika mfumo huo, maombi ya chombo hiki , yanatakiwa kupelekwa "Signis Service Rome". Na zaidi mfumo kama huo , huwa na manufaa pia, katika huduma zingine zinazotolewa na Signis.
Ombi kwa ajili ya kuruhusu utangazaji wa bure vipindi vya Redio Vatican, lipelekwe kwa maandishi kwa Giocomo Ghissan , Redio Vatican-Ofisi ya Uhusiano wa Kimataifa, kwa njia ya Fax , au Posta ya kawaida , pia mkipendekezwa lugha inayotaka kuchukua matangazao ya moja kwa moja kutoka Ibada za Kipapa.
Ofisi ya Uhusiano wa Kimataifa ya Redio Vatican, itatoa maelekezo yanayohusika na uunganishwaji katika njia za kusikiliza zilizounganishwa kupitia Internet- mfumo wa V-SAT , na utaratibu wake katika ufunguaji.
Radio Vaticana - International Relations Office
Dott. Giacomo Ghisani
Piazza Pia, 3
00120 - Citta del Vaticano
fax: (+39) 06.6988-3237
email : relint@vatiradio.va |
|
