HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t06

CTV - You tube

CTV



 home > Church > news


04/11/2009 10.11.37



Taarifa ya ziara ya mkaguzi wa kitume kwa mashirika ya kitawa nchini Marekani: matumaini na wasi wasi kwa siku za usoni!






Kardinali Franc Rodè, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na kazi za Kitume, katika taarifa yake baada ya kufanya hija ya kichungaji katika mashirika ya kitawa na kazi za kitume yaliyoko nchini Marekani, anasema, Baraza lake linapania kuhamasisha ari na mwamko wa miito ya maisha ya kitawa pamoja na kuboresha maisha ya watawa hao kwa siku za usoni.

Lengo la ziara hii ya kichungaji anasema Kardinali Rodè ni kutaka kutoa jibu muafaka baada ya kusikiliza maoni na kilio cha watu wa Mungu nchini Marekani kuhusu hali ya maisha ya Mashirika ya Kitawa na Kazi za kitume, kama yalivyobainishwa kwenye kongamano la kitawa lililofanyika kunako Mwezi Septemba, 2008. Wajumbe walibainisha changamoto toka kwa watu binafsi na kama zingefanyiwa kazi, zingeweza kuwa ni kwa ajili ya mafao ya Kanisa zima kwa ujumla.

Ziara hii ambayo tangu ilipotangazwa Mwezi Januari, 2009 imeleta hamasa kubwa miongoni mwa watu, itasaidia kupembua kwa kina hali halisi ya maisha ya watawa nchini Marekani pamoja na kutoa fursa kwa mtawa binafsi na jumuiya zao kufanya tafakari ya kina, kwani wakuu wa mashirika walihusika kwa karibu zaidi wakati wa ziara hii.

Wakuu wa Mashirika kwa hiyari yao wenyewe wameweza kushirikisha matumaini na wasi wasi waliyo nayo kwa Mama mkuu Mary Clare Millea, A.S.C.J., mkaguzi wa kitume. Mara tu baada ya hati ya kutendea kazi kutumwa kwa wakuu wa Mashirika anasema, Kardinali Franc Rodè, watawa waliomba muda wa sala binafsi na baadaye tafakari ambayo ingewashirikisha wanajumuiya wengine ndani ya Shirika. Awamu ya pili inatoa fursa kwa wakuu wa Mashirika kutoa taarifa inayoonesha hali halisi ya maisha ya kitawa kwa sasa na kwa siku za usoni.

Taarifa itatolewa hadharani, mara tu itakapokamilika, ili kubainisha mwelekeo wa maisha ya kitawa nchini Marekani kwa siku za usoni. Baraza la Kipapa halitatoa hitisho ya ziara hii hadi pale taarifa ya wakaguzi itakapokuwa imefanyiwa kazi. Kardinali Franc Rodè anaonesha matumaini na wasi wasi wake kwa maisha ya kitawa wakati huu na kwa siku za usoni nchini Marekani, hali ambayo inaweza kuathiri pia maeneo mengine duniani.

Kardinali Rodè anawaalika waamini na watu wenye mapenzi mema kuungana katika sala, ili ziara hii iweze kuzaa matunda yanayokusudiwa yaani kukoleza jitihada za kutoa utambulisho wa Kanisa Katoliki, katika maisha ya kitawa.


  « back to index

 






04/11/2009 15.36.45
Debate is necessary but the Truth must prevail, said Pope Benedict at the midweek General Audience.


04/11/2009 11.03.01
Benedikto XVI kuongoza Ibada ya kuwaombea marehemu Makardinali na Maaskofu Siku ya Alhamisi asubuhi


04/11/2009 9.49.31
Msalaba ni kielelezo cha upendo, umoja na huruma ya Mungu kwa watu wake! Si chanzo cha chuki na uhasama!


03/11/2009 11.47.24
"Wasindikizeni mapadre wenu kwa sala na sadaka katika hija yao ya utakatifu wa maisha"


03/11/2009 11.22.39
Lake Victoria - the next international symposium on Religion, Science and Environment.



Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top