04/11/2009 11.03.01


Benedikto XVI kuongoza Ibada ya kuwaombea marehemu Makardinali na Maaskofu Siku ya Alhamisi asubuhi


Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, siku ya alhamisi, tarehe 5 Novemba, 2009 saa tano na nusu saa za Ulaya anatarajiwa kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuwaombea marehemu Makardinali, Maaskofu wakuu na Maaskofu waliofariki dunia katika kipindi cha Mwezi Novemba, 2008 hadi kufikia Novemba 2009. Ibada hii itafanyika kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Taarifa kutoka Vatican inabainisha kwamba, kuna jumla ya Maaskofu ishirini na mbili walifariki dunia katika kipindi cha mwaka 2008. Idadi hii imeongezeka maradufu kwa mwaka 2009 kwani hadi kufikia tarehe 3 Novemba, 2009 kuna Maaskofu sabini na nane waliokwishafariki dunia.
Katika Ibada hiyo ya misa takatifu, Baba Mtakatifu atawakumbuka Makardinali saba na jumla ya Maaskofu mia moja. Raha ya milele uwape Ee Bwana na Mwanga wa Milele Uwaangazie, wapumzike kwa Amani. Amina.
|