HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t12

CTV - You tube

CTV



 home > Justice & Peace > news


05/11/2009 9.23.15



Mji wa Yerusalem hauna budi kuwa ni kitovu cha amani na suluhu ya migogoro katika Nchi Takatifu






Askofu mkuu Celestino Migliore, Mwakilishi wa kudumu wa Vatican kwenye Umoja wa Mataifa amesema, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Palestina, mwaka huu linaadhimisha miaka sitini tangu lilipoanzishwa, changamoto ya kukazia jitihada za kutafuta amani katika maeneo ya Palestina.

Askofu mkuu Migliore ameyasema hayo mapema wiki hii, alipokuwa anachangia mjadala katika kikao cha sitini na nne cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kinachoendelea Jijini New York. Kinzani na machafuko ya kisiasa Nchi Takatifu ni kielelezo cha wazi kabisa cha pande mbili zinazohusika kutotaka kuzingatia majadiliano na hatimaye kutafuta ufumbuzi wa kudumu juu ya mgogoro wa watu wa Palestina, ili kudumisha haki na amani eneo la Mashariki ya Kati.

Askofu mkuu Migliore ameiasa Jumuiya ya Kimataifa kuzidisha juhudi za majadiliano ili kumaliza uhasama na chuki baina ya pande hizi mbili. Mji wa Yerusalemu kama kielelezo cha amani, lazima uwe ni sehemu ya suluhu ya matatizo huko Nchi Takatifu, miongoni mwa pande hizi mbili zinazoendelea kusigana. Amani ya kudumu inayopata chimbuko lake katika moyo wa mwanadamu kwa njia ya majadiliano na wala si kwa kulazimishana itaweza kuzaa matunda yanayokusudiwa.


  « back to index

 






07/11/2009 11.47.03
"Jamii ya watanzania si takatifu wala kamilifu inaelemewa na dhambi ya kutotimiza wajibu"


07/11/2009 10.54.39
Imani thabiti ilichangia kuanguka kwa ukuta wa Berlini, miaka ishirini iliyopita!


05/11/2009 8.58.34
Mshikamano wa dhati, mafao ya kizazi kijacho na mabadiliko ya mtindo wa maisha; ni mambo ya kuzingatiwa katika agenda ya nishati


04/11/2009 13.06.37
Sheria ya watoto Tanzania kuhakikishia haki zao msingi


03/11/2009 8.29.27
Wakimbizi kutoka Burundi waanza kurudi nchi mwao, wanahitaji moyo wa uvumilivu na upendo ili kuijenga nchi yao kwa pamoja



Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top