HomeRadio Vaticana
foto testata  

Categories


  Charity & Solidarity


  Church


  Culture & Society


  Vatican Documents


  Synod


  Ecumenism


  Family


  Youth


  Justice & Peace


  Politics


  Religion & Dialogue


  Science & Ethics


  Audiences
   & Angelus



  Pastoral visits


cx_t17

CTV - You tube

CTV



 home > Pastoral visits > news


06/11/2009 10.42.34



Benedikto VXI jumapili ijayo kutembelea mji wa Brescia, alikozaliwa Papa Paulo wa sita, Baba wa Majadiliano!






Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita anasema, siri ya mafanikio katika shughuli za kichungaji zilizofanywa na Hayati Papa Paulo wa sita wakati wake, ni ule moyo wa kujitolea bila kujibakiza kwa ajili ya Kristo na Kanisa lake, akawa tayari hata kutoa maamuzi magumu na machungu. Upendo umekuwa uking'ara zaidi katika mafundisho yake ndani ya Kanisa.

Baba Mtakatifu jumapili ijayo tarehe 8 Novemba, 2009 anatarajiwa kufanya ziara ya kichungaji Jimboni Brescia kwa muda wa siku moja kwa kutembelea Brescia, Botticino na Concesio. Hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Jimbo la Brescia kumkaribisha Khalifa wa Mtakatifu Petro katika malango ya mji wake.

Hayati Baba Mtakatifu Yohane Paulo wa pili, alitembelea mji huu rasmi mara mbili, lakini pia kwa nyakati kadhaa alipata nafasi ya kuutembelea. Mara ya kwanza, ilikuwa ni mwaka 1982 alipokwenda kutoa heshima kwa mahali alipozaliwa Hayati Baba Mtakatifu Paulo wa sita pamoja na kufungua Taasisi ya Paulo wa sita.

Ziara ya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita Jimboni Brescia anasema Askofu Luciano Morati ni sehemu ya maadhimisho ya miaka thelathini, tangu alipofariki dunia Papa Paulo wa sita. Huu utakuwa ni muda wa sala na mshikamano na Khalifa wa Mtakatifu Petro, changamoto ya kukuza na kudumisha imani, upendo na matumaini. Ni fursa nyingine anasema Askofu Morati ya kudumisha umoja, upendo na uwajibikaji ili kuendelea kutambua dhamana na mchango wa kimissionari unaofumbatwa na waamini wa Jimbo la Brescia.

Waamini wa Brescia wamejiandaa kwa hija hii ya kichungaji kwa njia ya sala na katekesi. Asubuhi na mapema baada ya kuwasili, Baba Mtakatifu atakwenda kutoa heshima zake kwa Mtakatifu Arcangelo Tadini na baadaye ataelekea mjini Brescia kwenye Uwanja wa Paulo wa sita, ili kuwakumbuka watu nane waliopoteza maisha yao kutokana na vitendo vya kigaidi, kunako mwaka 1974. Ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu pamoja na kusali na waamini Sala ya Malaika wa Bwana.

Baada ya chakula cha mchana na mapumziko mafupi, Baba Mtakatifu ataelekea mjini Concesio ili kutembelea nyumba alimozaliwa Papa Montini pamoja na kukutana na familia ya Hayati Papa Paulo wa Sita na baadaye atafungua Makao Mapya ya Taasisi ya Paulo wa sita na baadaye atatembelea Kanisa alikobatizwa Papa Paulo wa sita. Baada ya tukio hilo anatarajiwa kurudi mjini Vatican.

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita daima ameendelea kumwelezea Hayati Papa Paulo wa sita kuwa ni zawadi ya Mungu kwa Kanisa lake, mfano na kielelezo cha utakatifu wa maisha ya kipadre. Ni mtu aliyekuwa na maono na mwelekeo mpana katika shughuli na mipango ya kichungaji kwa ajili ya Kanisa, akakuza na kuendeleza moyo wa umoja wa Kanisa, shughuli za kimissionari na majadiliano ya kiekukeme ili kudumisha umoja wa Kanisa.

Papa Paulo wa sita alijitahidi kuwa ni mfano bora wa kuigwa kwa ushuhuda wa maisha yake kwa kuonesha upendo kwa Kristo na Kanisa lake. Amejitahidi kuliongoza Kanisa kwa hekima na moyo wa kiinjili na mafundisho yake yataendelea kuacha chapa ya kudumu katika maisha na utume wa Kanisa, changamoto kwa waamini kufuata kwa uaminifu nyayo za Kristo.

Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita anasema, ukiangalia na kusoma kwa makini mafundisho ya Hayati Papa Paulo wa sita, utashangaa jinsi ambavyo yamepambwa kwa chapa ya upendo kwa Kristo na Kanisa lake. Anawaalika waamini na watu wenye mapenzi mema, kumsoma na kumwangalia Papa Paulo wa sita kwa jicho la upendo. Msukumo na mwelekeo wake wakati wa Mtaguso mkuu wa pili wa Vatican, umeliwezesha Kanisa kuwa na mwelekeo mpya katika nyakati hizi.

Papa Paulo wa sita kwa hakika, ni mtu aliyejitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya Kanisa mpaka dakika ya mwisho wa maisha yake, akiendelea kuwa jasiri na imara katika mafundisho yake. Ni mtu aliyependa majadiliano, jambo lililomwezesha kujenga misingi ya majadiliano ya kidini na kiekukemene, ili kuliwezesha Kanisa kuwa ni chombo cha majadiliano na kwa ajili ya huduma kwa binadamu, wanaokumbana na mahangaiko mbali mbali katika maisha, ili waweze kwa njia ya Kanisa kuonja matumaini mapya.

Kwa hakika wachunguzi wa mambo wanasema, ameliachia Kanisa utajiri mkubwa katika maisha na utume wake. Papa Paulo wa sita ni mtu aliyepambana na kifo kama binadamu, akiwa na imani katika maisha ya kikristo, hali akitambua kwamba, alikuwa pia ni Khalifa wa Mtakatifu Petro, jambo ambalo lilimdai ujasiri katika imani, matumaini na mapendo.


  « back to index

 






10/11/2009 8.19.40
Ziara ya Papa katika eneo la kuzaliwa Papa Paulo V1.





29/09/2009 14.53.33
Papa akamilisha ziara Czech


28/09/2009 15.29.32
Homilia na Ujumbe wa Papa kwa Vijana


28/09/2009 15.20.33
Papa akutana na dunia ya Wasomi- Praga



Related categories


Page précédente  Previous page
Page d'accueil  Home Page
Ecrire à la rédaction  Contact us
top
top
All the contents on this site are copyrighted ©. Webmaster / Credits / Legal Conditions
top
top